(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The books of 1 and 2 Samuel were originally one larger book simply known as âSamuelâ. It was first divided into two books in the Septuagint, which is the ancient Greek translation of the Old Testament. The books of 1 and 2 Samuel deal with the lives of Samuel the prophet, King Saul, and King David. Samuel was the final leader at the time when the nation of Israel changed from being ruled by judges to being ruled by kings. Samuel also anointed both Saul and David as the first two kings of Israel. The books of 1 and 2 Samuel give a historical description of the nation of Israel during that time.
No one knows who wrote 1 and 2 Samuel. The author didnât mention himself in the text, but he lived at least as late as the time of King David or probably much later and also had access to other documents about the lives of Saul and Samuel. Because of the mystery surrounding the author or authors of these books, it is also not known when they were written.
Outline of 1 Samuel:
1. Chapters 1-3 tell of the birth and calling of the prophet Samuel.
2. Chapters 4-7 describe how the Philistines took the ark of God from the Israelites and how it caused destruction in the lands of the Philistines while it was with them.
3. Chapters 8-15 tell what happened when the Israelites asked for a king and Samuel anointed Saul as the first king, and then later how the Lord rejected Saul.
4. In chapters 16-31 we read how Samuel anointed David as Israelâs second king and how Saul tried from then on to kill David.
Outline of 2 Samuel:
1. Chapters 1-5 describe how David became the king of Judah and then later also king of the rest of Israel.
2. Chapters 6-10 tell how David reigned as king and defeated many of his enemies.
3. In chapters 11-12 we read how David committed adultery and murder and was then rebuked by the prophet Nathan.
4. Chapters 13-20 tell of two different rebellions against David.
5. Chapters 21-24 make concluding remarks about Davidâs reign as king. ï»ż
Vitabu vya 1 Samweli na 2 Samweli mwanzoni vilikuwa ni kitabu kimoja kikubwa kilichojulikana kama âKitabu cha Samweliâ. Kwa mara ya kwanza kitabu hiki kiligawanywa na kuwa vitabu viwili katika toleo lililoitwa, âToleo la Septuagintiâ. Hili lilikuwa toleo la mwanzoni la tafsiri ya Agano la Kale katika lugha ya Kiyunani. Vitabu vya 1 Samweli na 2 Samweli vinabeba matukio ya kihistoria yanayohusu maisha ya nabii Samweli, mfalme Sauli, na mfalme Daudi. Samweli alikuwa ndiye kiongozi wa mwisho wakati taifa la Israeli lilipobadilika kutoka katika kutawaliwa na waamuzi, na kuanza kutawaliwa na wafalme. Samweli huyo huyo ndiye aliyewapaka mafuta Sauli na Daudi kuwa wafalme wa Israeli. Vitabu vya 1 Samweli na 2 Samweli vinatoa ufafanuzi wa kihistoria wa taifa la Israeli katika kipindi hicho.
Hakuna ajuaye ni nani aliyeviandika vitabu vya 1 Samweli na 2 Samweli. Mwandishi hakujitaja mwenyewe ndani ya vitabu hivyo, lakini yamkini alikuwa hai katika kipindi chote cha utawala wa mfalme Daudi, na pengine alisalia hai hata baada ya utawala huo, na yamkini pia alikuwa na uwezo wa kuona na kusoma nyaraka nyingine zilizoelezea maisha ya Sauli na Samweli. Kutokana na hali ya sintofahamu inayozunguka utambulisho wa mtu au watu walioandika vitabu hivi, pia haijulikani vitabu hivi viliandikwa lini.
Muhtasari wa Yaliyomo katika 1 Samweli:
1. Sura 1-3 zinasimulia kuzaliwa na kuitwa kwa nabii Samweli katika utumishi wa Mungu.
2. Sura 4-7 zinaelezea jinsi Wafilisti walivyolichukua sanduku la agano la Mungu kutoka kwa Waisraeli, na jinsi lilivyosababisha uharibifu katika miji ya Wafilisti wakatii lilipokuwa katika miji yao.
3. Sura 8-15 zasimulia jinsi Wasraeli walivyotaka wawe na mfalme; pia jinsi Samweli alivyompaka mafuta Sauli awe mfalme wa kwanza na jinsi Mungu alivyomkataa Sauli baadaye.
4. Katika sura 16-31 tunasoma jinsi Samweli alivyompaka mafuta Daudi awe mfalme wa pili wa Israeli na jinsi Sauli alivyojaribu hadi mwisho wa maisha yake kuyakatilia mbali maisha ya Daudi.
Muhtasari wa Yaliyomo katika 2 Samweli:
1. Sura 1-5 zaelezea jinsi Daudi alivyopata kuwa mfalme wa Yuda, na baadaye akawa mfalme wa Israeli yote.
2. Sura 6-10 zaelezea jinsi Daudi alivyotawala kama mfalme, na kuwashinda wengi wa adui zake.
3. Katika sura 11-12 twasoma jinsi Daudi alivyofanya dhambi ya uzinzi na kuua, na jinsi alivyokemewa na nabii Nathani.
4. Sura 13-20 zinasimulia uasi wa kwanza na wa pili ulioinuka dhidi ya Daudi.
5. Sura 21-24 zinatoa maelezo yanayohitimisha habari za maisha ya Daudi kama mfalme.
(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The book of Ruth tells of the wonderful events that happened to an Israelite family in the time of the Judges of Israel. The mother of this family, Naomi, faces great tragedy when her husband and two sons died while they were living in the foreign country of Moab. But then Naomi receives blessing when one of her daughters in law, Ruth, who is from the country of Moab, travels with her back to Israel and promises to support her. Then both Ruth and Naomi receive blessing when a family relative named Boaz, takes care of them and agrees to marry Ruth. The time of the Judges was bad and many Israelites lived with no regard for the law, but Naomi, Ruth, and Boaz are a good example of Israelites who follow Godâs laws.
No one knows who the author of Ruth was. The bookâs date of writing is also unknown, but some think it was written after Israelâs exile because of the type of Hebrew language used. It is significant that Ruth, who was not an Israelite, became the great-grandmother of King David. This also means that she is an ancestor of Jesus. This demonstrates that belonging to God is not just based on which family we belong, but on the heart.
Outline:
1. Chapter 1 tells of Naomiâs family and the tragedy they encountered and then how Naomi and Ruth returned to Israel.
2. In chapter 2 we read about how Ruth met Boaz while picking up leftover grain in his field.
3. Chapter 3 tells how Naomi sent Ruth to ask Boaz to marry her and take care of her because he was her close relative by marriage. Boaz then agrees to do this.
4. Chapter 4 describes how Boaz buys the property of Naomiâs dead husband and marries Ruth.
Kitabu cha Ruthu kinasimulia matukio ya kustaajabisha, yaliyoitokea familia moja ya Waisraeli katika kipindi cha Waamuzi wa Israeli. Naomi, Mama wa familia hii, anakabili kipindi cha msiba mkubwa wakati mumewe na wana wao wawili wa kiume walipofariki hali wakiwa ugenini katika nchi ya Moabu. Baada ya hayo, Naomi anapokea baraka baada ya Ruthu aliyekuwa mmoja wa wakweze na mwenyeji wa nchi ya Moabu kuamua kwa ridhaa yake mwenyewe kuambatana naye na kumsaidia. Naomi anaondoka na Ruthu akisafiri kurejea katika nchi yake mwenyewe ya Israeli. Baada ya hapo Ruthu na Naomi wote wanajikuta wakipokea baraka pale Boazi, mmoja wa jamaa wa karibu wa familia ya Naomi alipochukua jukumu la kuwatunza na kukubali kumwoa Ruthu. Kipindi cha Waamuzi kilikuwa kipindi kibaya kwa sababu Waisraeli walio wengi waliishi bila kuzingatia sheria, lakini Naomi, Ruthu na Boazi ni mfano mzuri wa Waisraeli walioishi kwa kuzingatia na kufuata sheria za Mungu.
Hakuna yeyote anayefahamu ni nani hasa aliyekiandika kitabu cha Ruthu. Tarehe ya kuandikwa kwa kitabu hiki pia haijulikani lakini wengi hudhani kwamba kitabu hiki kiliandikwa baada ya Waisraeli kutoka uhamishoni (utumwani) kutokana na aina ya Kiebrania kilichotumika katika uandishi wa kitabu chenyewe. Ni jambo lenye umuhimu mkubwa kwamba Mfalme Daudi alikuwa ni mjukuu wa Ruthu, mwanamke aliyekuwa si Muisraeli. Hii inamaanisha kwamba mwanamke huyu pia ana sehemu katika wahenga wa ukoo wa Yesu. Jambo hili linathibitisha ukweli kwamba kuhusiana na Mungu hakutokani na uteule wa kifamilia, bali hutegemea moyo wa mtu.
Muhtasari wa Yaliyomo:
1. Sura ya 1 inasimulia habari za familia ya Naomi na msiba mkubwa uliowapata, na kisha jinsi Naomi na Ruthu walivyorudi Israeli.
2. Katika sura ya 2 tunasoma jinsi Ruthu alivyokutana na Boazi alipokuwa anasimamia shughuli za uvunaji shambani mwake. Ruthu alikuwa anaokoteza masalia ya nafaka iliyobaki ndani ya shamba baada ya wavunaji kukusanya mavuno.
3. Sura ya 3 inasimulia jinsi Naomi alivyomwagiza Ruthu kumtaka Boaz amuoe na kumtunza kwa kuwa alikuwa jamaa yake wa karibu kutokana na mahusiano ya kindoa. Baada ya hapo Boazi anakubali kulitimiza jukumu hili.
4. Sura ya 4 inaelezea jinsi Boazi alivyonunua shamba lililokuwa milki ya marehemu mume wa Naomi, na kisha kumuoa Ruthu.
(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The book of Judges tells of Israelâs history after their initial conquest of the land of Canaan. It was a period of repeated rebellion and deliverance. The Israelites usually began to serve idols, and so God would raise up other nations to oppress them. Then the people would cry out and return to God, and so God would raise up leaders, called âjudges,â to lead and deliver the people from oppression.
No one is certain who the author of Judges is. Many traditionally believed that it was written by the prophet Samuel. We can be confident that this book was written during the time when Israel was ruled by a king. We believe this because the author refers to a time when Israel had no king (17:6, 18:1, 19:1, and 21:25). If the exodus of the Israelites from Egypt was around 1,400 B.C. (see the Introduction to the book of Exodus for more information) it would mean that the events of Judges occurred from around 1300 B.C. until 1050 B.C. when Saul became king.
Outline:
1. Chapters 1 through 3:6 tell of the final battles with the Canaanites after Joshua died. It also introduces the time of the judges when God raised up leaders who led and saved Israel.
2. Chapters 3:7 through 16:31 explain about the various judges God raised up to help Israel.
3. Chapters 17 through 21 speak of other rebellions of the Israelites.
Kitabu cha Waamuzi ni simulizi ya kipindi cha historia kilichofuata baada ya Waisraeli kuivamia na kuimiliki nchi ya Kanaani. Kilikuwa ni kipindi cha maasi kilichofuatiwa na vipindi vya adha, mateso, kukandamizwa, na kisha kuokolewa. Waisraeli kwa kawaida wangeanza kuabudu miungu ya sanamu, kisha Mungu angeinua mataifa mengine yaje na kuwakandamiza. Baada ya hapo watu wangelia na kumrudia Mungu, na hapo Mungu angeinua viongozi walioitwa âwaamuziâ, ili kuwaongoza watu na kuwatoa katika utumwa na maonevu.
Hakuna aliye na uhakika wa nani hasa aliyekiandika kitabu cha Waamuzi. Watu wengi kwa kufuata mapokeo fulani fulani waliamini kwamba nabii Samweli ndiye aliyekiandika. Twaweza kuwa na uhakika kabisa kwamba kiliandikwa katika wakati ambapo Israeli walikuwa tayari wana mfalme; kwa kuwa kitabu kinaangalia nyuma na kusema kuhusu nyakati za Waamuzi kwamba nyakati zile Israeli hawakuwa na mfalme (17:6, 18:1, 19:1, na 21:25). Ikiwa kama kipindi cha Waisraeli kutoka Misri kilitukia takribani kwenye mwaka 1400 K.K (angalia Utangulizi wa Kutoka kwa habari zaidi), basi inawezekana matukio ya Waamuzi yalitokea kati ya miaka ya 1300 hadi 1050 K.K wakati Sauli aliposimikwa kuwa mfalme wa Israeli.
Muhtasari wa Yaliyomo:
1. Sura 1 hadi 3:6 zasimulia habari za vita za mwishoni kati ya Waisraeli na Wakanaani baada ya kifo cha Yoshua. Pia zura hizi zinafungua pazia kutambulisha kipindi cha Waamuzi pale Mungu alipoinua viongozi walioongoza na kuwaokoa Israeli kutoka mikononi mwa adui zao.
2. Sura 3:7 hadi 16:31 zinaeleza habari za Waamuzi mbalimbali walioinuliwa na Mungu kuwasaidia Israeli.
3. Sura 17 hadi 21 zinaeleza habari za maasi mengine ya Waisraeli.
(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The book of Joshua continues the story of the nation of Israel where Deuteronomy stops. The people of Israel start on the east side of the Jordan River. The book of Joshua tells how they crossed the Jordan River and conquered the land of Canaan under the leadership of Mosesâ successor, Joshua. They did this because God commanded them. In this, God was fulfilling the promise that he had made to give the land Canaan to Abrahamâs descendants (Genesis 12:7).
It is not known who wrote or compiled the book of Joshua. At times, the author speaks as if he were there among the events that were taking place (for example, Joshua 5:1, 6). For this reason, many scholars think that Joshua wrote much of the book himself. However, it is clear that someone other than Joshua wrote certain sections, such as the description of Joshuaâs funeral (Joshua 24:29). Other scholars believe that the book was written about 800 years after the events happened. The events in the book of Joshua likely happened around 1 250 B.C., which would have been 40 years after Rameses ruled in Egypt. Rameses is the king who is thought to have ruled during the time of Israelâs exodus from Egypt (Exodus 1:11).
Outline:
1. Chapters 1 through 5:12 tell how the Israelites crossed the Jordan River and entered into the land of Canaan.
2. Then, chapters 5:13 through 12 tell of Israelâs conquest of Canaan.
3. Next, chapters 13-21 describe how the land of Canaan was divided up among the tribes of Israel.
4. Finally, chapters 22-24 tell how some of the tribes returned to the Eastern side of the Jordan River, of Joshuaâs farewell and funeral, and how Israelâs covenant with God was renewed.
Kitabu cha Joshua kinaendeleza simulizi ya kihistoria ya taifa la Israeli kikianzia pale kitabu cha kumbukumbu kinapoishia. Wakati kitabu cha Yoshua kikianza simulizi yake, Waisraeli wamepiga kambi upande wa mashariki wa mto Yordani. Kitabu hiki kinaelezea jinsi walivyouvuka mto huo na kuwashinda wenyeji wa nchi ya Kanaani wakiwa chini ya uongozi wa Yoshua aliyemrithi Musa kama kiongozi wa taifa. Walifanya hivyo kwa sababu ndivyo Mungu alivyowaamuru wafanye. Katika hili, Mungu alikuwa anaitimiza ahadi aliyoitoa kwamba angewapa wazawa wa Abrahamu nchi ambayo kwanza ilikaliwa na Wakanaani (Mwanzo 12:7).
Haijulikani ni nani aliyekiandika na kukipangilia kitabu cha Yoshua. Katika baadhi ya nyakati, mwandishi anamfanya mtu mwingine ahisi kana kwamba mwenyewe alikuwa mshiriki wa matukio yaliyokuwa yanatokea (kwa mfano, Yoshua 5:1, 6). Kutokana na sababu hii, wasomi wengi wa mambo ya Biblia hudhani kwamba Yoshua mwenyewe ndiye aliyeandika sehemu kubwa ya kitabu chenyewe. Ni wazi pia kwamba mtu mwingine tofauti na Yoshua aliandika baadhi ya sehemu za kitabu hiki, kwa mfano yale maelezo ya msiba na mazishi ya Yoshua (Yoshua 24:29). Wasomi wengine wanaamini kwamba kitabu kiliandikwa yapata kama miaka 800 baada ya tukio lenyewe. Matukio yanayotajwa ndani ya kitabu cha Yoshua yamkini yalitokea katika mwaka wa 1250 K.K., takribani kama miaka 40 baada ya Farao Rameses kuanza kuitawala Misri. Huyu Rameses ndiye mtawala anayefikiriwa kuwa aliitawala Misri katika wakati Israeli walipokuwa wanatoka Misri (Kutoka 1:11).
Muhtasari wa Yaliyomo:
1. Sura 1 hadi 5:12 zasimulia jinsi Waisraeli walivyovuka mto Yordani na kuingia ndani ya nchi ya Kanaani.
2. Kisha, sura 5:13 hadi 12 zasimulia habari za harakati za Waisraeli kuivamia Kanaani.
3. Baada ya hapo, sura 13-21 zinaelezea jinsi nchi ya Kanaani ilivyogawanywa kwa makabila yote ya Israeli.
4. Hatimaye, sura 22-24 zasimulia jinsi baadhi ya makabila yalivyorudi upande wa mashariki ya mto Yordani; maneno ya buriani ya Yoshua kwa taifa; kifo na mazishi yake pamoja na jinsi Waisraeli walivyoadhimisha kumbukumbu ya agano lao na Mungu.
(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The book of Deuteronomy is a repetition of the laws found in the rest of the books of the Pentateuch (the first five books of the Old Testament). In Hebrew, the bookâs name means âWordsâ. It is generally believed that Moses wrote the book of Deuteronomy except for the very end which recounts his death. The book begins by saying that âthese are the words Moses spoke to all Israel.â The idea that Moses is the author of Deuteronomy is also supported several times in the New Testament. One example is found in Acts 3:22-23 where Peter quotes Deuteronomy 18:15-18 and states that these were Mosesâ words. Moses would have written Deuteronomy, as well as Genesis, Exodus, Leviticus, and Numbers about 1 300 or 1 400 years B.C.
Deuteronomy was written like a treaty between a king and another kingdom under his authority, as it was done in ancient times. It is an agreement between God and the people of Israel. God agreed to bless the people if they would follow his laws. If Israel was disobedient to Godâs laws, they would be punished. This is a theme throughout the book, but chapters 27 and 28 especially emphasize it by listing specific blessings and curses which would result from Israelâs obedience or disobedience. The different tribes of Israel stood on two different mountains while they spoke these blessings and curses at each other in a loud voice to confirm the covenant.
Outline:
1. In chapters 1 through 3 Moses recounts what happened during Israelâs travels through the wilderness.
2. Chapters 4 through 26 explain the requirements of the covenant between God and his people.
3. Then in chapters 27 through 30 the Israelites speak the blessings and curses in a loud voice to show that the covenant was official.
4. Lastly, in chapters 31 through 34 Moses speaks some final words to Joshua and each tribe of Israel before his death.
Kitabu cha Kumbukumbu la Torati ni marudio ya sheria zinazoelezwa kutolewa ndani ya vitabu vingine vya Torati (vitabu vitano vya kwanza katika Agano la Kale). Jina la Kiebrania la kitabu hiki lina jina lenye maana ya âManenoâ. Kwa jumla, inaaminika kwamba Musa ndiye aliyekiandika kitabu hiki isipokuwa kisehemu kifupi cha mwishoni kinachoelezea kifo chake. Kitabu hiki kinaanza kwa maneno yasemayo, âHaya ndiyo maneno Musa aliyowaambia Israeli.â Wazo kwamba Musa ndiye aliyekuwa mwandishi wa Kumbukumbu la Torati linathibitishwa mara kadhaa katika Agano Jipya. Mfano mmoja unakutikana katika Matendo 3:22-23 katika sehemu ambapo Petro ananukuu Kumbukumbu 18:15-18 na kutamka kwamba haya yalikuwa ni maneno ya Musa. Musa aweza kuwa alikiandika kitabu cha Kumbukumbu la Torati, pamoja na vitabu vya Mwanzo, Kutoka, Walawi, na Hesabu kati ya miaka ya 1400 au 1300 K.K. (kabla ya Kuzaliwa kwa Kristo).
Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kiliandikwa mithili ya mkataba kati ya mfalme na ufalme mwingine ulio chini ya mamlaka yake, kama ilivyofanyika katika enzi za kale. Ni mkataba kati ya Mungu na watu wa Israeli. Mungu alikubali kuwabariki watu endapo kama wao wangefuata na kutii sheria zake. Endapo kama Israeli wangeasi amri za Mungu, basi wangeadhibiwa. Hii ndio mada kuu katika kila eneo la kitabu hiki, lakini hasa sura 27 na sura 28 inamsisitizo wa ukweli huu ikiorodhesha baraka maalumu na laana ambazo zingetokana na utii au uasi wa taifa la Israeli. Makabila tofauti ya Israeli yalisimama katika milima tofauti iliyosimama mkabala, na wakatamkiana baraka hizo na laana kama njia ya kulithibitisha agano kwamba waliliafiki.
Muhtasari wa Yaliyomo:
1. Katika sura 1 hadi 3 Musa anakumbusha yaliyotokea katika safari ya Israeli kuvuka jangwa.
2. Sura 4 hadi 26 zinaelezea masharti ya agano kati ya Mungu na watu wake.
3. Kisha katika sura 27 hadi 30 watu wa Israeli wanatamka baraka na laana kwa sauti kubwa kuonyesha kwamba tokea wakati huo agano lilikuwa limerasimishwa.
4. Mwishowe, katika sura 31 hadi 34 Musa anazungumza maneno ya kutamatisha kwa Joshua, na kwa kila kabila la Israeli kabla ya kifo chake.
(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The book of Numbers tells about Israelâs journey of 40 years through the wilderness before they reached the promised land, Canaan. The book is called Numbers because it has two sections that show the number of fighting men in each tribe of Israel (chapter 1 and chapter 26). Traditionally, scholars believe that the book of Numbers, as well as the other books in the Pentateuch (Genesis, Exodus, Leviticus, and Deuteronomy), were written by the prophet Moses. This seems to be suggested by the text itself because Numbers starts by saying that God spoke to Moses (Numbers 1:1). It is also possible that Moses wrote most of the book and that scribes later added some parts. For example: it is difficult to think that Moses would have written a verse like Numbers 12:3, where his own humility is praised.
During their journey through the wilderness, the Israelites complained and rebelled against God several times. In response, they were punished. One example of this is when the Israelites were afraid and complained that the people of Canaan were too strong (Numbers 14:1–4). Because of this, God said that a whole generation of people would die before the Israelites could enter the promised land. Moses himself also disobeyed God and was not allowed to go into the promised land. And even though the people rebelled, God continued to protect them. When the Israelitesâ enemies hired a pagan seer called Balaam to speak curses on the Israelites, God only allowed him to speak blessings on them instead (Numbers 22-24).
Outline:
1. Chapters 1 through 10:11 contain information about a census of the Israelites, as well as the arrangement of their camp, the priestsâ duties, and the gifts that were received from each tribe when the altar was dedicated.
2. Then Numbers tells about Israelâs journey through the wilderness, in chapters 10:12 through 25.
3. Chapters 26 through 36 describe the second census and other instructions for the nation of Israel. This includes the names of places where the Israelites had set up camp on their way to the promised land and how this land would be divided among the tribes when they entered it. ï»ż
Kitabu cha Hesabu kinaelezea safari ya miaka 40 ya wana wa Israeli kupitia jangwani, walipokuwa hawajaingia ndani ya nchi ya ahadi, yaani nchi ya Kanaani. Kitabu chenyewe kinaitwa Hesabu kwa sababu kina sehemu mbili zinazotoa idadi ya wanaume wapiganaji waliokuwamo katika kila kabila la Israeli (sura 1 na 26). Kimapokeo, wanazuoni wa mambo ya kibiblia wanaamini kwamba kitabu cha Hesabu, na pia vitabu vingine vilivyomo ndani ya Torati (Mwanzo, Kutoka, Walawi, na Kumbukumbu la Torati), viliandikwa na nabii Musa. Ukweli huu unadokezwa na kitabu chenyewe kwa kusema Mwenyezi Mungu aliongea na Musa (Hesabu 1:1). Yawezekana pia kwamba Musa aliandika sehemu kubwa ya kitabu chenyewe, na waandishi wengine wakaongeza baadhi ya sehemu katika miaka iliyofuata baadaye. Kwa mfano, ni vigumu kufikiria kwamba Musa angeweza kuwa aliandika aya kama ya Hesabu 12:3, mahali ambapo unyenyekevu wake mwenyewe ulisifiwa.
Katika safari yao ya jangwani, wana wa Israeli walinungâunika na kumuasi Mungu mara kadhaa. Kutokana na vitendo vyao hivyo, waliadhibiwa. Mfano mmoja wa jambo hili ni wakati wana wa Israeli walipoogopa na kulalamika kwamba Wakanaani walikuwa na nguvu sana kuliko wao (Hesabu 14:1-4). Kutokana na tendo hili, Mungu alisema kwamba kizazi chote cha watu kingekufa kabla wana wa Israeli hawajaingia ndani ya nchi ya ahadi. Ilifikia hata Musa mwenyewe akakosa kumtii Mungu, na kutokana na hili hata yeye hakuweza kuingia ndani ya nchi ya ahadi. Japokuwa watu waliasi, lakini Mungu aliendelea kuwalinda. Wakati maadui wa watu wa Israeli walipomkodisha nabii wa kipagani aliyeitwa Balaamu atamke laana juu ya watu wa Israeli, Mungu alimruhusu tu atamke baraka juu yao (Hesabu 22-24).
Mhutasari wa Yaliyomo:
1. Sura 1 hadi 10:11 zimebeba habari zinazohusisha sensa ya wana wa Israeli, pia kuna mpangilio wa kambi yao ulivyokuwa, majukumu ya makuhani, na matoleo yaliyokusanywa kutoka katika kila kabila wakati madhabahu na hema la ibada vilipowekwa wakfu.
2. Baada ya hapo kitabu cha Hesabu kinaelezea safari ya Watu wa Israeli kupitia jangwani, katika sura 10:12 hadi 25.
3. Sura 26 hadi 36 inaelezea sensa ya pili na maelezo mengine kwa ajili ya taifa la Israeli. Hii ni pamoja na majina ya sehemu ambako watu wa Israeli waliweka kambi wakiwa safarini kuelekea katika nchi ya ahadi, na jinsi ambavyo nchi hiyo ingegawanywa kati ya makabila yote watakapokuwa wameingia ndani ya nchi yao wenyewe.
(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The book of Leviticus is made up of laws which God gave the Israelites through Moses. These laws concern the offering of sacrifices and regulating worship in the tabernacle. The word Leviticus means âregarding the Levitesâ who were the tribe in Israel chosen by God to be priests and to look after the temple. Traditionally, scholars believe that the book of Leviticus, as well as the other books in the Pentateuch (Genesis, Exodus, Numbers, and Deuteronomy), was written by the prophet Moses. This seems to be suggested by the text itself, because Leviticus starts by saying that God spoke these words to Moses (Leviticus 1:1). Others believe that this book may have been compiled from ancient documents in the 5-6th century B.C. in Babylon.
In the beginning of the book of Leviticus, we read about several kinds of sacrifices which God commanded that the priests should offer. Some of these sacrifices were made for people’s sins. Other sacrifices could be given voluntarily because of a personâs love for God. In every case, it was important for the sacrifice to be the best that a person could give, without any imperfection. This clearly showed Godâs holiness. The last part of the book explains how Israelites and the priests could remain ritually pure or become ritually pure. The main theme of the book is that God is holy and that by following the laws in this book, the Israelites could live in Godâs presence.
Outline:
1. Chapters 1 through 7 give commands on how to perform the various sacrifices.
2. Chapters 8 through 10 tell how Aaron and his sons were appointed as priests.
3. Chapters 11 through 16 give laws about pure and impure foods as well as diseases.
4. Chapters 17 through 27 describe many other commands concerning matters like eating, celebrations, moral behavior, and Sabbath years.
Kitabu cha Walawi ni mkusanyiko wa sheria walizopewa watu wa Israeli na Mungu kupitia Musa. Sheria hizi zinahusu mfumo wa utoaji wa dhabihu na sadaka. Pia sheria hizi zinatoa mfumo, kanuni, na taratibu za ibada ndani ya hema ya kukutania. Neno Walawi kama lilivyoandikwa katika lugha ya asili limebeba maana ya âyahusuyo Walawiâ. Watu waliokuwa ndio kabila teule la Mungu lenye jukumu la kuendesha shughuli za kikuhani na kazi ya utunzaji wa hekalu. Kulingana na mapokeo, wanazuoni wa mambo yahusuyo Biblia huamini kwamba kitabu cha Walawi, pamoja na vitabu vingine vya Torati (Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Kumbukumbu la Torati), viliandikwa na nabii Musa. Ukweli huu unadokezwa pia na maandiko ya kitabu chenyewe, kwa sababu kitabu cha Walawi kinaanza kwa kusema kwamba âMwenyezi Mungu alimwita Musa na kuongea naye katika hema la mkutano..â(Walawi 1:1). Wengine huamini kwamba yamkini kitabu hiki kiliandikwa kama mkusanyo wa nyaraka kadhaa za kale katika karne ya 5-6 K.K. (Kabla ya Kuzaliwa kwa Kristo), wakati wana wa Israeli walipokuwa uhamishoni (utumwani) Babeli.
Mwanzoni mwa kitabu cha Walawi, tunasoma kuhusiana na aina kadhaa za sadaka na dhabihu Mungu alizoamuru zitolewe na makuhani. Baadhi ya dhabihu hizi zilitolewa kama kafara kwa ajili ya malipizi ya dhambi za watu. Dhabihu zingine ziliweza kutolewa kutokana tu na upendo wa waliozitoa kwa Mungu wao. Katika hali zote hizo, lilikuwa jambo la muhimu sana kwa sadaka anayoitoa mtu iwe katika kiwango cha hali ya juu sana ya ubora, isiyo na kasoro yoyote au kilema. Ni ukweli ulio dhahiri kwamba kanuni hii ilidhihirisha utakatifu na ukamilifu wa Mungu. Katika sehemu ya mwisho ya kitabu hiki, inaelezwa jinsi watu wa Israeli pamoja na makuhani walivyoweza kusalia katika hali ya utakatifu au kujitakasa pale ambapo tatizo lilikuwa limetokea. Mada kuu ya kitabu hiki ni kwamba Mungu ni mtakatifu na kwa kuzifuata sheria zilizo ndani ya kitabu hiki, watu wa Israeli wangeweza kuishi ndani ya uwepo wa Mungu.
Muhtasari wa Yaliyomo:
1. Sura 1 hadi 7 inatoa maamrisho na namna ya kutoa dhabihu na sadaka mbalimbali.
2. Sura 8 hadi 10 inaelezea jinsi Haruni na wanawe walivyoteuliwa na kufanywa makuhani.
3. Sura 11 hadi 16 inaelezea sheria zihusuzo vyakula vilivyo safi na vilivyo najisi, pia magonjwa.
4. Sura 17 hadi 27 inafafanua maamrisho mengine yanayohusu sheria nyingine nyingi zihusuzo mambo kama ulaji, sherehe, mwenendo wa kimaadili, na miaka ya Sabato.
(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The book of Exodus continues the history of Abrahamâs family line, that started in Genesis. The word Exodus means âexitâ, referring to the nation of Israelâs exit from Egypt to return to the country which God had promised to Abraham. Traditionally, scholars believe that most of the book of Exodus was written by the prophet Moses, and this seems to be suggested by the text itself. Exodus 24:4 tells how Moses wrote down parts of the book. In Joshua 8:31 it refers to a command in Exodus 20:25 and says that it was âwritten in the Book of the Law of Moses.â The New Testament refers to books written by Moses several times, for example when speaking about what happened at the burning bush and saying that it was written in âthe book of Mosesâ (Mark 12:26). The exit of the Israelites from Egypt likely took place around about 1,300 or 1,400 years B.C.. In 1 Kings 6:1 it says that the exodus took place 480 years before the 4th year of Solomonâs reign as king over Israel.
Exodus emphasizes how God was keeping his promise to Abraham, Isaac, and Jacob. It tells about Godâs mighty deliverance of Abrahamâs descendants, the nation of Israel, from the land of Egypt. From there God led his people to the foot of mount Sinai where he gave Moses many laws for the Israelites to follow. These laws outline how they should act, how they should make sacrifices, and detailed instructions for constructing the tabernacle (which was to be Godâs dwelling place among them), the ark and other equipment for worship at the tabernacle, and the priestsâ special clothes. Then after a terrible rebellion where Israel had made a golden idol in the form of a calf, Moses met with God again. In the final part of the book, we read how the items outlined earlier were constructed.
Outline:
1. Chapter 1 explains how the Israelites had been enslaved in the country of Egypt.
2. Chapters 2-4 introduce Moses and tell about his life up to the time when he was called to deliver Godâs people.
3. Then the writer explains how God produced mighty wonders and plagues in Egypt in order to deliver his people from that land and from Pharaohâs army (chapters 5-15:21).
4. From here the nation of Israel travelled to Mount Sinai (chapters 15:22-19).
5. In chapters 20-31 we read how God gave Moses the Law, which contained detailed instructions for how Godâs people, the Israelites, had to live and worship.
6. In chapter 32 it is written how the Israelites rebelled against God by convincing Mosesâ brother Aaron to make an idol in the form of a golden calf.
7. Chapters 33-40 tell how Moses saw Godâs glory and then instructed the Israelites about Godâs Law and how to make the tabernacle, the ark and other equipment for worship at the tabernacle, and the priestsâ special clothes.
Kitabu cha Kutoka kinaendeleza simulizi ya kihistoria iliyoanzia katika kitabu cha Mwanzo ikihusu historia ya ukoo wa Abrahamu. Neno Exodus lililotafsiriwa kama Kutoka lina maana ya kupenya katikati ya malango na kwenda nje, likielezea kitendo cha taifa la Israeli cha kuponyoka kutoka katika utumwa wa Misri na kurudi katika nchi ambayo Mungu alikuwa amemwahidi Abrahamu. Kulingana na mapokeo, wanazuoni wanaamini kwamba sehemu kubwa ya kitabu hiki iliandikwa na nabii Musa, na jambo hili hata linashuhudiwa na kitabu chenyewe. Kutoka 24:4 yaelezea jinsi Musa alivyoandika baadhi ya sehemu za kitabu hiki. Kifungu katika Yoshua 8:31 kinataja amri iliyoko katika kitabu cha Kutoka 20:25, na kusema, âkama ilivyoandikwa katika Kitabu cha torati ya Musa.â Vitabu vya Agano Jipya vinataja mara kadhaa na kunukuu vitabu vilivyoandikwa na Musa, kwa mfano Agano Jipya linapoeleza habari za kichaka kilichowaka moto pasipo kuteketea, linaelezea kwamba habari hii iliandikwa ndani ya âkitabu cha Musaâ (Marko 12:26). Yaelekea kwamba kitendo cha Wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri kilitokea katikati ya miaka 1,300 au 1,400 K.K (Kabla ya Kristo). Katika kitabu cha 1 Wafalme 6:1 imetajwa kwamba kitendo cha kutoka kilifanyika yapata miaka 480 kabla ya mwaka wa 4 wa kutawala kwake Sulemani kama mfalme wa Israeli.
Kitabu cha Kutoka kinatoa msisitizo wa namna ambayo Mungu alitenda ili kudumisha uaminifu wake juu ya ahadi alizokuwa amewaahidi Abrahamu, Isaka na Yakobo. Kitabu kinasimulia kuhusu matendo makuu ya ukombozi wa Mungu kwa wana wa Abrahamu ambao ndio taifa la Israeli, walipokuwa wakitoka katika nchi ya Misri. Kutoka huko Mungu aliwaongoza watu wake hadi katika tambarare zilizokuwa chini ya mlima Sinai mahali ambapo Mungu alimpa Musa sheria nyingi ili Waisraeli wazifuate. Sheria hizi zinaelezea jinsi ilivyowapasa kutenda, jinsi walivyotakiwa kutoa dhabihu (sadaka), na maelezo ya kina yaliyohusu ujenzi wa hema ya kukutania (mahali ambapo ndipo palipokuwa pawe makao ya Mungu katikati yao), pia sanduku la agano na vifaa vingine kwa ajili ya ibada ndani ya hema la ibada, na nguo maalumu kwa ajili ya makuhani. Kisha mara baada ya tukio la uasi mbaya pale wana wa Israeli walipojitengenezea sanamu ya ngâombe wa dhahabu, Musa alikutana na Mungu tena. Katika sehemu za mwishoni za kitabu hiki, tunasoma jinsi vifaa vilivyotajwa awali vilivyotengenezwa.
Muhtasari:
1. Sura ya 1 yaelezea jinsi wana wa Israeli walivyotiwa utumwani nchini Misri.
2. Sura 2-4 zinamtambulisha Musa na kusimulia maisha yake kutoka utotoni hadi pale alipoitwa kuwakomboa watu wa Mungu.
3. Kisha mwandishi anasimulia jinsi Mungu alivyofanya maajabu na kuipiga nchi ya Misri kwa mapigo makuu kwa lengo la kuwakomboa watu wake kutoka katika nchi ile, na pia kutoka katika kitisho cha jeshi la Farao (sura 5-15:21).
4. Kutoka hapa taifa la Israeli lilisafiri na kufika katika eneo la Mlima Sinai (sura 15:22-19).
5. Katika sura 20-31 tunasoma jinsi Mungu alivyompa Musa Torati, sheria iliyokuwa na maelezo ya kina yaliyoelekeza jinsi watu wa Mungu, Waisraeli, walivyopaswa kuishi na kuabudu.
6. Katika sura ya 32 imeandikwa jinsi wana wa Israeli walivyomuasi Mungu pale walipomshawishi ndugu wa Musa aliyeitwa Haruni awatengenezee sanamu iliyokuwa na umbo la ngâombe wa dhahabu.
7. Sura 33-40 zaelezea jinsi Musa alivyouona utukufu wa Mungu, na kuwafundisha Waisraeli sheria za Mungu, pamoja na kuwaelekeza jinzi ya kujenga hema ya kukutania, sanduku la agano na vifaa vingine vya ibada katika hema ya kukutania, na mambo muhimu yahusuyo mavazi maalumu ya makuhani.