(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The word Genesis means âbeginningâ and it is the first book in the Old Testament of the Bible. The original Hebrew even starts with the words âIn the beginning.â It shows where everything came from and especially how Godâs dealings with humans began. Scholars today have several theories about the person or persons who wrote Genesis and also about when it was written. Some believe that it may have been compiled from ancient documents in the 5-6th century B.C. in Babylon. Others accept the traditional belief that Moses wrote Genesis, as well as Exodus, Leviticus, Numbers, and Deuteronomy about 1,300 or 1,400 years B.C.
Genesis contains very important information that helps Christians to understand the rest of the Bible, both the Old and New Testaments. It shows us how sin entered the world and peopleâs need for a savior. It also reveals Godâs plan to save people. This can be seen from the first prophecy about Jesus (Genesis 3:15) and Godâs promise to Abraham to bless all nations on the earth (Genesis 12:3).
Outline:
1. God created the world and Adam and Eve, as told in chapters 1 and 2.
2. Chapters 3 through 5 describe Adam and Eve, their sin, and their descendants.
3. Chapters 6 through 9 tell about Noah and the great flood.
4. Then the book of Genesis describes what happened between the time of Noah and the time of Abraham, including the tower of Babel, in chapters 10 and 11.
5. Chapters 12 through 50 are about Abraham, his family, and the start of the nation of Israel.
a. The lives of Abraham and his wife Sarah are covered in chapters 12 through 25.
b. The lives of Isaac and his wife Rebekah are covered in chapters 21 through 28, and his death is described in chapter 35.
c. The lives of Jacob, his sons, and their move from Canaan to Egypt are covered in chapters 25 through 50.
d. Chapters 37 through 50 focus on the life of Jacobâs favorite son Joseph and how he became a ruler in Egypt. ï»ż
Neno asilia linalobeba jina la kitabu hiki Genesis lina maana ya âmwanzoâ na hivyo ndivyo kitabu hiki cha kwanza cha Agano la Kale kinavyoitwa. Nakala asilia ya Kiebrania ya kitabu hiki pia inaanza na meneno âHapo mwanzo.â Kitabu hiki kinatuonyesha pahala vitu vyote vilikotoka, na jinsi Mungu alivyoanza kuhusiana na wanadamu. Wanazuoni siku hizi wana nadharia nyingi tofauti kuhusu mtu au watu waliokiandika kitabu cha Mwanzo, na ni wakati gani kitabu hiki kiliandikwa. Wapo wanaodhani kwamba kitabu hiki kiliandikwa kikitokana na nyaraka za kale katika kipindi cha kati ya karne ya 5 - 6 K.K. (Kabla ya Kuzaliwa Kristo). Wengine wanakubaliana na mapokeo yanayokubalika kati ya watu walio wengi kwamba Musa aliandika kitabu cha Mwanzo, na pia vitabu vingine ambavyo ni Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu, na Kumbukumbu la Torati Katikati ya miaka ya 1,300 au 1,400 K.K).
Kitabu cha Mwanzo kimesheheni habari zilizo za muhimu sana zinazowasadia Wakristo kuzielewa sehemu nyingine zote zilizosalia za Biblia, ziwe ni za Agano la Kale au Jipya. Kitabu cha Mwanzo kinatuonyesha jinsi dhambi ilivyoingia ulimwenguni, na jinsi watu wote wanavyomuhitaji Mkombozi. Kitabu hiki pia kinauweka wazi mpango wa Mungu wa kuwaokoa watu. Hili linaweza kudhihirika kutokana na unabii wa kwanza unaotabiri kumhusu Yesu (Mwanzo 3:15), na ahadi ya Mungu kwa Abrahamu ya kuyabariki mataifa yote yaliyoko duniani (Mwanzo 12:3).
Muhtasari:
1. Mungu aliuumba ulimwengu, na pia akawaumba Adamu na Hawa kama inavyosimuliwa katika sura ya 1 na ya 2.
2. Sura ya 3 hadi ya 5 inawaelezea Adamu na Hawa, dhambi yao, na uzao wao.
3. Sura ya 6 hadi ya 9 inamwelezea Nuhu na habari za ile gharika kuu.
4. Baada ya hapo kitabu cha Mwanzo kinaelezea kile kilichotokea katikati ya kipindi cha Nuhu na kile cha Abrahamu, ikijumlisha pia habari za mnara wa Babeli katika sura ya 10 na 11.
5. Sura ya 12 hadi ya 50 zinamhusu Abrahamu, familia yake na mwanzo wa taifa la Israeli.
a. Maisha ya Abrahamu na mkewe Sara yanaelezewa kutoka katika sura ya 12 hadi ya 25.
b. Maisha ya Isaka na mkewe Rebeka yanaelezewa kutoka katika sura ya 21 hadi ya 28, na kifo chake kinasimuliwa katika sura ya 35.
c. Maisha ya Yakobo na Esau, wanawe Isaka, yanasimuliwa katika sura ya 25 hadi ya 50.
d. Sura ya 37 hadi ya 50 imesheheni habari za mwana kipenzi wa Yakobo, na jinsi alivyokuja kufanywa mtawala wa nchi ya Misri.