(Pioneer Bible Translators and The Word for the World use the following introduction in many of their translation projects around the world.)
The book of Judges tells of Israelâs history after their initial conquest of the land of Canaan. It was a period of repeated rebellion and deliverance. The Israelites usually began to serve idols, and so God would raise up other nations to oppress them. Then the people would cry out and return to God, and so God would raise up leaders, called âjudges,â to lead and deliver the people from oppression.
No one is certain who the author of Judges is. Many traditionally believed that it was written by the prophet Samuel. We can be confident that this book was written during the time when Israel was ruled by a king. We believe this because the author refers to a time when Israel had no king (17:6, 18:1, 19:1, and 21:25). If the exodus of the Israelites from Egypt was around 1,400 B.C. (see the Introduction to the book of Exodus for more information) it would mean that the events of Judges occurred from around 1300 B.C. until 1050 B.C. when Saul became king.
Outline:
1. Chapters 1 through 3:6 tell of the final battles with the Canaanites after Joshua died. It also introduces the time of the judges when God raised up leaders who led and saved Israel.
2. Chapters 3:7 through 16:31 explain about the various judges God raised up to help Israel.
3. Chapters 17 through 21 speak of other rebellions of the Israelites.
Kitabu cha Waamuzi ni simulizi ya kipindi cha historia kilichofuata baada ya Waisraeli kuivamia na kuimiliki nchi ya Kanaani. Kilikuwa ni kipindi cha maasi kilichofuatiwa na vipindi vya adha, mateso, kukandamizwa, na kisha kuokolewa. Waisraeli kwa kawaida wangeanza kuabudu miungu ya sanamu, kisha Mungu angeinua mataifa mengine yaje na kuwakandamiza. Baada ya hapo watu wangelia na kumrudia Mungu, na hapo Mungu angeinua viongozi walioitwa âwaamuziâ, ili kuwaongoza watu na kuwatoa katika utumwa na maonevu.
Hakuna aliye na uhakika wa nani hasa aliyekiandika kitabu cha Waamuzi. Watu wengi kwa kufuata mapokeo fulani fulani waliamini kwamba nabii Samweli ndiye aliyekiandika. Twaweza kuwa na uhakika kabisa kwamba kiliandikwa katika wakati ambapo Israeli walikuwa tayari wana mfalme; kwa kuwa kitabu kinaangalia nyuma na kusema kuhusu nyakati za Waamuzi kwamba nyakati zile Israeli hawakuwa na mfalme (17:6, 18:1, 19:1, na 21:25). Ikiwa kama kipindi cha Waisraeli kutoka Misri kilitukia takribani kwenye mwaka 1400 K.K (angalia Utangulizi wa Kutoka kwa habari zaidi), basi inawezekana matukio ya Waamuzi yalitokea kati ya miaka ya 1300 hadi 1050 K.K wakati Sauli aliposimikwa kuwa mfalme wa Israeli.
Muhtasari wa Yaliyomo:
1. Sura 1 hadi 3:6 zasimulia habari za vita za mwishoni kati ya Waisraeli na Wakanaani baada ya kifo cha Yoshua. Pia zura hizi zinafungua pazia kutambulisha kipindi cha Waamuzi pale Mungu alipoinua viongozi walioongoza na kuwaokoa Israeli kutoka mikononi mwa adui zao.
2. Sura 3:7 hadi 16:31 zinaeleza habari za Waamuzi mbalimbali walioinuliwa na Mungu kuwasaidia Israeli.
3. Sura 17 hadi 21 zinaeleza habari za maasi mengine ya Waisraeli.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.